ARTURO VIDAL AIPONGEZA CHILE KWA KUTETEA TAJI COPA AMERICA



ARTURO VIDAL AIPONGEZA CHILE KWA KUTETEA TAJI COPA AMERICA
STAA Arturo Vidal amekipongeza kikosi cha timu ya taifa ya Chile, baada ya kufanikiwa kutetea vyema taji lake la Copa America kwa mikwaju ya penati dhidi ya Argentina.

 Hatua hiyo ya penati ilifikiwa baada ya kushindwa kufungana hadi muda wa nyongeza na huku kila timu ikiwa imebaki na wachezaji 10, Chile wakafanikiwa kuondoka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya Lionel Messi na Lucas Biglia kukosa mikwaju yao kwa upande wa Argentina.

Wakati Vidal akiwa ameshakosa penati yake ya kwanza kwa upande wa Chile, ilishuhudiwa Nicolas Castillo, Charles Aranguiz, Jean Beausejour na Francisco Silva wakaipatia ushindi timu yao.

"Ilikuwa mechi ngumu kwa timu ya taifa ambayo ni nzuri," alisema Vidal.

"Lakini jambo la muhimu ni kwamba tumeshindana kufanikiwa kufikia malengo yetu," aliongeza nyota huyo.


Alisema kuwa kikosi kinachounda timu hiyo mara zote kimekuwa kikifurahisha kwa ubora.


Comments