KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameapa kuinasa saini ya kiungo wa Leicester City, N'Golo Kante hasa baada ya kuikosa saini ya mshambuliai wa timu hiyo, Jamie Vardy.
Wenger aliyasema hayo baada ya kujiondoa kwenye mbio za kuwania saini ya Vardy Alhamisi iliyopita wakati nyota huyo alipoamua kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kuongeza mkataba wa miaka minne.
Kwa sasa Wenger mwenye umri wa miaka 66, atajaribu kurusha karata nyingine kwa nyota mwingine wa timu hiyo akidai kuwa Kate yuko miongoni mwa nyota wanaowaniwa na klabu hiyo.
Comments
Post a Comment