Lionel Messi ameifikia rekodi ya Gabriel Batistuta (Bat Goal) ya kuwa mfungaji wa wakati wote kwa timu ya taifa ya Argentina baada ya kuifungia timu yake bao na kufikisha mabao 54. Messi aliiongoza Argentina kuichapa Venezuela mbao 4-1 na kufuzu nusu fainali kwa kupambana na wenyeji Marekani.
Argentina walianza kujipatia ushindi dakika ya 8 tu pale Gonzalo Huguain alipopachika mpira kimiani kufuatia pande safi alilomegewa na Messi. Dakika 20 baadaye yaani dakika ya 28 Gonzalo Huguain akaipatia timu yake bao la pili. Mnamo dakika ya 43 mwamuzi Roberto Orozco akawazawadia Venezuela penati, ambapo mchezaji Seijas alipiga kwa staili ya "Panenka il Cucchiais" lakini kipa wa Argentina Romelo aliishitukia na kutulia pale pale na kuidaka.
Dakika ya 60 ndipo 'Rapulga' Lionel Messi akaifungia timu yake bao la 3. Venezuela walijipatia goli la kifuta chozi dakika ya 70 kupitia kwa nyota wake Solomoni Rondon, goli ambalo halikudumu hata dakika 1 kwa dakika ya 71 Lamela akaipatia Argentina bao la 4.
Nako kwenye dimba la Levis Stadium,Santa Clara Califonia, Chile walimpa Mexico mapumziko ya wiki yaani goli 7-0.Alikuwa mchezaji hatari wa Chile Eduardo Vargas aliyeingia kimiani mara 4, dakika ya 15, 51, 56 na 73.Huku Edson Puch akifunga goli 2, dakika ya 44 na 86, naye Alexis Sanchez akifunga goli moja dakika ya 48. Sasa Chile atapambana na Colombia katika hatua ya nusu fainali.
Comments
Post a Comment