STRAIKA wa klabu ya Atletico Madrid na Ufaransa, Antoine Griezmann amesema ana uhakika kuwa kiungo Paul Pogba ana uwezo mkubwa wa kuwa mchezaji bora wa dunia.
Griezmann aliongeza kuwa nyota huyo wa klabu ya Juventus atakuwa msaada mkubwa kwa taifa la Ufaransa katika kuhakikisha wanatwaa Kombe la Euro litakalofanyika kwenye ardhi yao.
"Ana nguvu na ubunifu mkubwa sana, kasi na uwezo kubwa wa kupiga mashuti, nafikiri Pogba ana kila sifa ya kuwa nyota wa dunia," alisema Griezmann.
Comments
Post a Comment