WILLIAM GALLAS AMTAKA CONTE KUINUSURU CHELSEA



WILLIAM GALLAS AMTAKA CONTE KUINUSURU CHELSEA
BEKI wa zamani wa Chelsea William Gallas amemtaka kocha mpya wa klabu hiyo, Antonio Conte kuinusuru klabu baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu uliopita ambapo ilishindwa kutetea ubingwa wake na kumaliza ikiwa nafasi ya kumi.

Aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho ndie aliyetolewa kafara kwa kufukuzwa Desemba mwaka jana, kabla ya Guus Hiddink kuinusuru isishuke daraja.

Conte ndie atakaeinoa klabu hiyo ya tanford Bridge baada ya kuiongoza Italia kwenye michuano ya fainali za Mataifa ya Ulaya Uero 2016 na Gallas ambaye amewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili akiwa na Chelsea katika kipindi cha 2001 na 2006 alichoitumikia ana matumaini kocha huyo wa zamani wa Juventus ataiwezesha kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi.

"Ni vigumu mno kuinoa Chelsea ikiwa kwenye nafasi kama hii hususan katika kipindi cha miaka mitano niliyokuwa mahali hapo," beki huyo wa zamani wa Ufaransa aliuambia mtandao wa Omnisport.


"Lakini inaweza ikatokea kwa klabu kubwa kama hii, nadhani msimu ujao utakuwa mwingine, nina matumaini tutaiona Chelsea ikiwa kileleni," alisema staa huyo wa zamani.


Comments