LEICESTER City imetwaa kwa mara ya kwanza taji la Premier League bila kushuka dimbani baada ya mechi kati ya Chelsea na Tottenham kumalizika kwa sare ya 2-2, lakini hiyo haikuwa historia pekee iliyoandikwa Stamford Bridge Jumatatu usiku.
Bali matokeo hayo yalikwenda sambamba na Spurs kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza katika historia ya Premier League wachezaji wake tisa kulimwa kadi za njano katika mechi moja na kushangaza zaidi kwa kukosekana hata mmoja wa kutolewa nje kati yao!
Kutoka dakika 27 hadi 51 tayari nyota wanne walilimwa kadi, mmoja mwingine akipewa kadi kati ya mabao mawili ya Chelsea na wanne zaidi baada ya Eden Hazard kufunga bao la kusawazisha dakika 83, ambapo watatu kati yao katika dakika za majeruhi.
Nyota wa Spurs waliolimwa kadi za njano ni Kyle Walker (dk 27), Jan Vertonghen (dk 38), Danny Rose (dk 45), Erik Lamela (dk 51), Christian Eriksen (dk 70), Eric Dier (dk 88), Harry Kane (dk 90), Moussa Dembele (dk 90) na Ryan Mason (dk 90).
Comments
Post a Comment