STAA Thiago Alcantara ameelezea dhamira yake ya kubaki Bayern Munich licha ya kuendelea kuwepo na tetesi zinazodai kwamba ataondoka na kocha wake, Pep Guardiola atakapokwenda Manchester City.
Guardiola ndie aliyempeleka Thiago Bayern akitokea Barcelona wakati kocha huyo alipoanza kuinoa klabu hiyo ya Allianzarena mwaka 2013 na sasa kuna tarifa zinazodai kwamba anataka kuwa na staa huyo mwenye umri wa miaka 25 kwenye kikosi chake kipindi atakapoanza kibarua chake kipya katika michuano hiyo ya Ligi Kuu England.
Hata hivyo, mapema mwaka huu Thiago alikanusha taarifa hizo za kwamba anataka kuitema klabu hiyo ya mabingwa wa Ligi ya Bundesliga na tena juzi kupitia katika mitandao ya kijamii akarudia kauli yake hiyo ya kwamba ataendelea kuitumikia.
"Nawashukuru kwa msaada wenu, tutaonana msimu ujao," aliandika kupitia mtandao wake wa Twitter.
Comments
Post a Comment