SCHOLES AMPIGIA DEBE GIGGS KWA MOURINHO



SCHOLES AMPIGIA DEBE GIGGS KWA MOURINHO
STAA wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes ni kama anampigia debe nyota mwenzake wa zamani, Ryan Giggs, baada ya kusema kwamba ana matumaini atakuwemo kwenye jopo la wafanyakazi wa Jose Mourinho wakati atakapokuwa akiinoa klabu hiyo ya Old Trafford.

Mourinho ndie aliyemrithi Louis Van Gaal katika kitimoto cha klabu hiyo ya Old Trafford baada ya Mholanzi huyo kufukuzwa zikiwa ni siku mbili tangu aiwezeshe Manchester United kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.

Giggs alikuwa msaidizi wa Van Gaal katika kipindi cha miaka miwili na alikuwa akitajwa kuwa ndie angekabidhiwa timu hiyo mwaka 2017 ambao kocha huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa amepanga kuondoka lakini Mourinho anadaiwa kuwa ataajiri wafanyakazi wake akiwemo mshirika wake wa karibu, Rui Faria.


Hali hiyo ndiyo inayoweka shakani kibarua cha Giggs na huku ripoti nyingine zikidai kwamba mshindi huyo mara 13 wa mataji ya Ligi Kuu anaweza kutafuta kibarua kwingine.


Comments