SAFARI IMEWADIA!!! LOUIS VAN GAAL ASEMA 'IT'S OVER'


SAFARI IMEWADIA!!! LOUIS VAN GAAL ASEMA 'IT'S OVER'
Louis van Gaal anaonekana kama vile anakiri kuwa muda wake wa kuwa kocha wa Manchester United umefika ukingoni baada kuondoka London huku akiwaambia waandishi wa habari 'it's over' (imekwisha/imefika mwisho).

Licha ya kushinda taji la FA kwa ushindi wa  2-1 katika mchezo ulioenda hadi 'extra time' dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi, hatma ya kocha huyo iliingia mashakani kwa mara nyingine tena muda mfupi tu baada ya mchezo huo uliochezwa Wembley. 

Mwandishi wa Sky Sports James Cooper aliyekuwepo nje ya hotel ya Hilton katikati ya London walikofikia Manchester United, anafichua kuwa Van Gaal alipoulizwa kuhusu hatma yake alijibu: "No, no. It's over!".

BBC imedai Jose Mourinho atatangazwa kuwa kocha mpya wa Manchester United ndani ya siku chache zijazo.
Louis van Gaal appeared to suggest he was leaving                  United before arriving back in Manchester by trainĀ 
Louis van Gaal akiondoka jiji la London kurejea Manchester baada ya mchezo wa fainali ya FA




Comments