Ni ukweli usiofichika kwamba Anthony Martial ni moja ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa sana katika msimu huu wa EPL.
Kinda huyo wa raia wa Ufaransa alijiunga na Manchester United kwa ada ya paundi milioni 36 akitokea klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Watu wengi waliutilia shaka uhamisho wake, wakidai kwamba amegharimu kiasi kikubwa cha fedha ukilinganisha na umri wake bila ya kusahau changamoto zilizopo Ligi Kuu England. Lakini haikuchukua hata mwezi Martial kuwaziba midomo walimtilia mashaka.
Kwa ufupi tu, tuangazie takwimu ambazo zinathibitisha dhahiri shahiri kwamba Martial tayari ni mchezaji mkubwa kwenye Ligi ya England.
- Amekuwa mfungaji bora wa Man United katika msimu wake wa kwanza
- Amevunja rekodi
Amevunja rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi kijana kuwahi kusajiliwa katika historia ya klabu ya Manchester United. Amekuwa mchezaji wa kwanza chini ya miaka 20 kununuliwa kwa paundi milioni 36.
3. Amefunga goli la kihistoria
- Uwezo wa kuzoea mazingira kwa haraka
- Anaweza kuwa na ubora zaidi ya Cristiano Ronaldo
Comments
Post a Comment