Robert Lewandowski            anaweza kuwa njiani kuondoka Bayern Munich kiangazi hiki baada            ya wakala wake kubainisha kuwa kuna maongezi yameanza ya            mchezaji huyo na Real Madrid.
        Mshambuliaji huyo            ambaye kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Poland inayojiandaa            na michuano ya Euro 2016, alikuwa nguzo kuu katika kuiwezesha            Bayern kutwaa taji la Bundesliga            kwa mwaka wa nne mfululizo akifunga magoli 30 na kuwa mchezaji            wa kwanza asiye raia wa Ujerumani kufanya hivyo.
        Baada ya kutumia            muda wake mwingi kucheza soka la kulipwa Ujerumani, nyota huyo            mwenye umri wa miaka 27, hakufanya siri utashi wake kutaka            kusaka changamoto mpya nje ya Bundesliga            na sasa wakala wake Cezary Kucharski  anazidi kuchagiza hatua hiyo kwa kufichua            kuwa Real Madrid tayari wamebisha hodi kusaka huduma ya mteja            wake.
        Robert Lewandowski              njiani kutua Real Madird
        
Comments
Post a Comment