BEKI wa timu ya              taifa ya Ufaransa, Raphael Varane ameachwa kwenye kikosi cha              timu ya taifa ya nchi hiyo.
        Varane              hajajumuishwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ijayo              ya Euro itakayoanza mwezi Juni kutokana na kusumbuliwa na              majeraha ya nyama za paja.  
        Pia nyota huyo wa              klabu ya soka ya Real ameukosa mchezo wa fainali ya Kombe la              klabu bingwa Ulaya uliopigwa leo kati ya timu yake na              Atletico Madrid.
        Mchezaji huyo              atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu hadi nne na              nafasi yake kwenye kikosi cha taifa imechukuliwa na beki wa              Adil Rami, mwenye umri wa miaka 30 anayechezea timu ya              Sevilla ya nchini Hispania.
        
Comments
Post a Comment