PEP GUARDIOLA ATAMBIA UBORA BAYERN MUNICH



PEP GUARDIOLA ATAMBIA UBORA BAYERN MUNICH
KOCHA anayeondoka Bayern Munich, Pep Guardiola, amesema amekuwa kocha bora zaidi katika misimu mitatu ndani ya klabu hiyo, wakati ambapo anajiandaa kucheza mechi yake ya mwisho kwenye Ligi Kuu ya Ujerumani "Bundesliga".

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona ambaye ameshinda Ligi ya Bundesliga katika miaka yake mitatu, anajiunga na mancheste City ya England msimu ujao.

"Nimejifunza mengi kutoka kwa wachezaji wangu. Ninafurahia uamuzi wangu wa kuja hapa."

Mechi ya jana kati ya Bayern Munich na Hannover ndiyo iliyokuwa ya mwisho katika katika uwanja wa Allianza Arena kwa Mhispania huyo.


Mechi yake ya mwisho itakuwa ya Kombe la Ujerumani dhidi ya BorussiaDortmund wiki ijayo, huku akitarajia kushinda taji la pili katika kipindi cha miaka mitatu.


Comments