MOURINHO KUFANYA KUFURU YA USAJILI MANCHESTER UNITED ...kupewa jeuri ya pauni mil 200, nyota kibao kwenda Old Trafford




MOURINHO KUFANYA KUFURU YA USAJILI MANCHESTER UNITED ...kupewa jeuri ya pauni mil 200, nyota kibao kwenda Old Trafford

Kocha ajae Manchester United, Jose Mourinho anategemewa kufanya mageuzi makubwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa usajili wa wachezaji nyota utakaoigharimu timu hiyo takriban pauni milioni 200 katika msimu huu wa usajili.

Mourinho anayeenda kuchukua mikoba ya Louis van Gaal aliyetimuliwa Jumatatu, amewakeka katika orodha yake sentahafu John Stones wa Everton na kiungo wa Chelsea Nemanja Matic.

Stone anatarajiwa kuigharimu Manchester United pauni milioni 45 wakati Matic anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.

Mourinho pia anampigia hesabu beki wa Real Madrid Raphael Varane mwenye thamani ya pauni milioni 45 pamoja na kiungo bab kubwa wa Sporting Lisbon ya Ureno Joao Mario kwa pauni milioni 35.

Kama vile hiyo haitoshi, Mourinho anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya United kwa kumulika wachezaji kadhaa akiwemo muuaji mkongwe wa PSG Zlatan Ibrahimovic,  Alvaro Morata wa Juventus, Higuain Gonzalo wa Napoli na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.
Incoming Manchester United boss Jose Mourinho is                  keen to sign his former Chelsea midfielder Nemanja                  Matic
Kocha ajae Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo  Nemanja Matic wa Chelsea
Mourinho is also keen on Everton and England                  defender John Stones, who he has tried to sign in the                  past 
Mourinho anamtaka kwa udi na uvumba beki wa Everton na England  John Stones, ambaye alijaribu kumsani bila mafaniko msimu uliopita
Former                  Chelsea boss Mourinho was pictured near his London home                  with Rui Faria on Monday afternoon
Kocha wa zamani wa  Chelsea Jose Mourinho katika picha iliyopigwa Jumatatu huko London akiwa na Rui Faria 


Comments