Manchester City iko mbioni kushinda vita vya kuwania saini ya kiungo mkongwe wa Arsenal anayeelekea kutundika daluga.
City inataka kumnasa nyota huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 34 ili akawe kocha msaidizi wa Pep Guardiola.
Mara baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu baina ya Arsenal na Aston Villa, Arteta aliweka wazi kuwa ana ofa tatu mkononi za benchi la ufundi ikiwemo ya kwenda Machester City.
Mikel Arteta (katikati) akilia baada ya mchezo wake wa mwisho kwa Arsenal Jumapili iliyopita
Mikel Arteta akifarijiwa na wachezaji wenzake
Ofa zingine za ukocha usaidizi ambazo Arteta hakutaka kuzitaja zinahusishwa na Arsenal na Tottenham, lakini inaaminika kuwa tayari City imepiga hatua kubwa mbele katika dili hilo.
Comments
Post a Comment