Michael Carrick anaamini Jumanne usiku katika uwanja wa Old Trafford, alicheza mchezo wake wa mwisho kwa Manchester United kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 alisindikizwa na watoto wake, Jacey na Louise, wakati alipoiongoza United kuingia uwanjani kwenye mchezo wao wa mwisho wa Premier League msimu huu dhidi ya Bournemouth.
Rio Ferdinand na Patrice Evra nao pia walisindikizwa na watoto wao katika mchezo wa mwisho Old Trafford, ishara inayoonyesha kuwa Carrick naye anaweza akatimka United baada ya fainali ya FA dhidi ya Crystal Palace Jumamosi huu.
United bado haijaonyesha nia ya kumbakiza Carrick kwa kile kinachoaminika kuwa inataka kuwekeza kwa vijana zaidi. Arsenal na Newcastle zinatajwa kuwania saini ya kiungo huyo iwapo ataachwa na Manchester United.
Kiungo Michael Carrick anaamini mwisho wake Manchester United umewadia
Carrick (kushoto) na Wayne Rooney ndiyo watumishi wa muda mrefu waliosalia kwenye kikosi cha United
Comments
Post a Comment