KINDA wa Manchester City raia wa Nigeria, Kelechi Iheanacho amekiri kuwa amejifunza mengi kutoka kwa kinda mwenzake wa Manchester United, Marcus Rashford msimu huu na mkutakia mafanikio katika maisha yake ya soka.
Makinda hao mastraika ambao wamekuwa wakilinganishwa uwezo, wameng'ara msimu huu na klabu hizo pinzani za Jiji la Manchester, wakionyesha ubora wa hali ya juu katika kuzifumania nyavu.
Rashford, Muingereza mwenye miaka 18 amepiga mabao saba katika mechi 16 akiwa na United, huku Iheanacho mwenye miaka 19 akifunga 13 katika mechi 34 alizoichezea City.
Iheanacho amevutiwa na Rashford tangu alipoibuka Februari mwaka huu, na amekiri kuwa amejifunza mengi kutoka kwake na anaamini atakuwa mchezaji mkubwa Old Trafford.
"Rashford ni kipaji kichanga cha hali ya juu. Ni "mkubwa", madhubuti na anafanya maamuzi mazuri, hivyo nadhani anaelekea kuwa mchezaji mzuri wa United miaka ijayo," alisema Iheanacho kuliambia gazeti la Daily Mail.
Akizungumzia kulinganishwa na Rashford, alisema ni changamoto nzuri kwa sababu inampa hamasa na ujasiri zaidi wa kupambana.
Comments
Post a Comment