MATUTA YAIPA REAL MADRID UBINGWA CHAMPIONS LEAGUE


MATUTA YAIPA REAL MADRID UBINGWA CHAMPIONS LEAGUE
Ramos pumps his fists            in delight after breaking the deadlock at the San Siro much to            the delight of his Real Madrid team-mates
Real Madrid imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuwanyoa watani zao Atletico Madrid kwa njia ya matuta.

Hatua hiyo ya matuta ilikuja baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120 za mchezo.

Katika mikwaju ya penalti Real Madrid ikaibuka na ushindi wa 5-4.

Real Madrid ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 5 kupitia kwa Sergio Ramos bao lililodumu hadi dakika ya 79 pale Yannick Ferreira-Carrasco alipoisawazishia Atletico.



Comments