KIUNGO Mario Gotze amerejea mazoezini katika timu ya taifa ya Ujerumani baada ya kupona tatizo lake la kuvunjika mfupa wa ubavuni.
Kutokana na majeraha hayo, kiungo huyo mshambuliaji wa Bayern Munich alilazimika kuikosa mechi ya fainali ya Kombe la Ujerumani DFB – Pokal, lakini juzi akarejea kwenye kikosi cha Ujerumani kilichopo nchini Uswisi kwa ajili ya kujiandaa na mechi mbili za maandalizi ya fainali za Mataifa ya Ulaya (Euro 2016), dhidi ya Slovakia na Hungary.
Gotze alijikuta katika kipindi kigumu Bayern katika muda wa mwisho wa Pep Guardiola kwenye klabu ya Allianzarena na licha ya Carlo Ancelotti kuwa ndie atakayeinoa kuanzia msimu ujao, kuna taarifa zinazodai kwamba atakwenda kuungana na kocha wake wa zamani wakati akiwa Borussia Dortimund, Jurgen Klopp anayeinoa Liverpool.
Akizungumza kuhusu Gotze katika mkutano wa waandishi wa habari juzi, kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Roy alisema kwamba aliwasiliana na staa huyo wiki iliyopita na akameleza kila kitu kuhusu hali ya afya yake.
Comments
Post a Comment