MANCHESTER UNITED YAPIGWA BAO LA KISIGINO NA CHELSEA …Barcelona na Bayern vinara wa kuuza jezi duniani



MANCHESTER UNITED YAPIGWA BAO LA KISIGINO NA CHELSEA …Barcelona na Bayern vinara wa kuuza jezi duniani
Manchester United            estimate that making do with the Europa League next season            will cost them £40million
CHELSEA imeipiga kumbo Manchester United katika mauzo ya jezi miongoni mwa klabu za Premier League msimu wa 2015/16, huku ikishika nafasi ya tatu duniani, licha ya kusuasua na kushindwa kutetea ubingwa.

Mauzo ya jezi za Chelsea yamepanda kwa asilimia 39 kutoka msimu uliopita na kufikia jezi 3,102,000, ikiwa ni asilimia 5 zaidi ya mauzo ya United iliyofanikiwa kuuza jezi 2,977,000. Arsenal inakamata nafasi ya tatu kwa klabu za England na ya saba duniani ikiuza jezi 2,055,000.

Kwa mujibu wa wakala wa masoko ya vifaa vya michezo, Euroamericas, Barcelona ndiyo kinara barani Ulaya ikiuza jezi 3,637,000, ikifuatiwa na Bayern Munich iliyouza jezi 3,312,000.

Kuendelea kufanya vizuri kwa Atletico Madrid iliyofanikiwa kuingia fainali ya Champions League kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu, kumeifanya kuingia kumi bora kwa mara ya kwanza kwa kuuza jezi 1,977,000 idadi ambayo imeiwezesha kushika nafasi ya nane.

VINARA 10 WA KUUZA JEZI 2015/16
1. Barcelona: Mil. 3,637,000
2. Bayern Munich: Mil. 3,312,000
3. Chelsea: Mil. 3,102,000
4. Man Utd: Mil. 2,977,000
5. Real Madrid: Mil. 2,866,000
6. PSG: Mil. 2,212,000
7. Arsenal: Mil. 2,055,000
8. Atletico Madrid: Mil. 1,977,000
9. Juventus: Mil. 1,678,000

10. AC Milan: Mil. 1,287,000


Comments