MANCHESTER UNITED YAMALIZIA KIPORO CHAKE KWA USHINDI ...RASHFORD ATAKATA, ROONEY AFUNGA BAO LA 100 OLD TRAFFORD
Manchester United imeichapa AFC Bournemouth 3-1 katika wa mwisho wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Old Trafford Jumanne usiku.
Matokeo ya mchezo huo ambao uliopaswa kufanyika Jumapili na kuahirishwa baada ya tishio la kuwepo bomu kwenye uwanja huo, hayajabadili chochote katika mbio za kusaka tiketi ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Wayne Rooney aliifungia United bao la kwanza dakika ya 43 akimalizia kazi nzuri ya Anthony Martial. Hilo linakuwa ni bao la 100 la Premier League kwa nahodha huyo wa England na Manchester United katika uwanja huo wa Old Trafford.
Akicheza mchezo wa kwanza tangu aitwe timu ya taifa ya England, kinda Marcus Rashford akaifungia United goli la pili kunako dakika ya 75 kabla ya Ashley Young hajafunga goli la tatu ilipotimu dakika ya 87.
United imemaliza katika nafasi ya tano na sasa itacheza michuano ya Europa League msimu ujao.
MANCHESTER UTD (4-1-4-1): De Gea 6; Valencia 7, Smalling 6.5, Blind 6, Borthwick-Jackson 6.5; Carrick 7; Lingard 6, Mata 6 (Herrera 75'), Rooney 7.5, Martial 6.5 (Young 83'); Rashford 7 (Depay 78').
BOURNEMOUTH (4-4-2): Federici 6.5; Francis 6.5, Elphick 6, Cook 6, Daniels 7; Ritchie 6, Gosling 6, Surman 5.5, Pugh 7 (Gradel 66, 6); King 6.5 (Afobe 66, 6), Wilson 6.5 (Grabban 79).
Wayne Rooney akishangilia bao lake la 100 kwenye uwanja wa Old Trafford katika Premier League
Nahodha wa England akiifungia United bao la kwanza dakika ya 43 kufuatia pasi ya Anthony Martial
Marcus Rashford (katikati), aliyecheza mchezo wake wa kwanza Manchester United tangu alipochaguliwa kwenye kikosi cha England kwaajili ya Euro 2016, akishangilia bao lake
Winga aliyetokea benchi Ashley Young (katikati) akifunga kwa kuunganisha krosi tamu ya Rooney
Hivi ndiyo Msimamo wa ligi ulivyo
Comments
Post a Comment