MANCHESTER United sasa inasubiri miujiza kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya England baada ya kukubali kichapo cha bao 3-2.
Kabla ya mchezo wa huo wa kiporo uliochezwa Jumanne usiku kwenye dimba la Upton Park, United ilikuwa na matumaini ya kumaliza katika nafasi ya tatu, lakini sasa imebakiwa na nafasi finyu ya kushika nafasi ya nne.
United yenye pointi 63 sasa italazimika kushinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya AFC Bournemouth Mei 15 halafu iombe Manchester City yenye pointi 65 ifungwe na Swansea City, kinyume na hapo, klabu hiyo ya Old Trafford itajikuta ikiambulia nafasi ya kucheza Europa League msimu ujao huku Champins League ikiota mbawa kwao.
West Ham ilikuwa ya kwanza kufunga katika dakika ya 10 kupitia kwa Diafra Sakho bao lililodumu hadi mapumziko.
Anthony Martial akaifungia United mabao mawili katika dakika ya 58 na 72 na kuifanya West Ham ikicharuke na kupata magoli yaliyokuja dakika ya 76 na 81 yaliyofungwa na Michail Antonio na Winston Reid.
Comments
Post a Comment