MANCHESTER UNITED NA RENATO SANCHES WA BENFICA KINAZIDI KUELEWEKA


MANCHESTER UNITED NA RENATO SANCHES WA BENFICA KINAZIDI KUELEWEKA

Manchester United ni kama vile imeshamnyakua kiungo  wa Benfica  Renato Sanches kwa dili la pauni milioni 63 kwa.

United ilikuwa kwenye maongezi ya kina tangu mwezi Januari kwaajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ambapo  rais wa Benfica Luis Filipe Vieira alikwenda Manchester siku 1o zilizopita kwaajili ya kukamilisha maongezi ya dili hilo.

Sanches yupo Benfica kwa mkataba wa hadi mwaka 2021 na ana kipengele kinachomruhusu kuondoka kwa pauni milioni 60, lakini inaaminika vilabu hivyo vimekubaliana malipo ya pauni milioni 31.5 mwanzoni na nusu ilibakia italipwa baadae kadri ya nyota huyo atakavyokuwa bora katika utumishi wake ndani ya Manchester United.

Luis Filipe Vieira alikuwa katika jiji la Manchester siku 1o zilizopita
Kiungo huyo ameichezea Benfica mechi 22 msimu huu na kufunga magoli mawili huku akiitwa timu ya taifa na kuichezea mechi mbili..
Inaaminika Sanches ndiyo kipaji kipya cha kipekee Ureno kinchokuja baada ya Cristiano Ronaldo.
Jumapili usiku Sanches alilambwa kadi nyekundu wakati Benfica ikishinda 2-0 dhidi ya Maritimo huku ikidhaniwa kuwa huo ni mchezo wake wa mwisho kwa Benfica kabla hajaelekea Old Trafford.


Comments