MANCHESTER UNITED KUMTANGAZA JOSE MOURINHO WIKI IJAYO KAMA KOCHA WAO MPYA


MANCHESTER UNITED KUMTANGAZA JOSE MOURINHO WIKI IJAYO KAMA KOCHA WAO MPYA
Jose Mourinho is reportedly set to become Manchester            United's new manager

Manchester United inajipanga kumtangaza Jose Mourinho kama kocha wao mpya wiki mapema wiki ijayo, hii ni kwa mujibu wa Shirika la habari la Uingereza - BBC.

Kwa mujibu wa BBC, ni kwamba kocha huyo mwenye umri wa miaka 53, kimsingi alishakubaliana na United hata kabla ya mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace uliochezwa Jumamosi.

Kwa United chini ya  Louis van Gaal kushindwa kunasa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, klabu hiyo ya Old Trafford inaamini sasa ni wakati muafaka wa kufanya mabadiliko. 

Mourinho amekuwa hana kazi tangu alipotimuliwa na Chelsea mwezi Disemba.

BBC inasema United imepanga kutangaza ujio wa Mourinho mapema wiki ijayo pindi tu watakapomwambia Van Gaal, 64 kuwa huduma yake ndani ya Old Trafford imefikia kikomo.







Comments