MATAJIRI wa jiji la Manchester, Manchester City, wameweka jina la mlinzi wa Bayer Leverkusen, Lukas Boeder katika orodha ya wachezaji wanaowawania katika usajili wa majira ya kiangazi.
Kwa mujibu wa Daily Mail, City inapambana na klabu nyingine nyingi zinazowania saini ya mlinzi huyo, ikiwemo Barcelona.
Lakini City imetajwa kuwa katika mkakati mzuri wa kumnasa Rolfes ikiwa ni azma ya kukiimarisha kikosi cha msimu ujao.
Boeder amekuwa katika kiwango kizuri kwa miaka miwili iliyopita na kuwa tegemeo katika kikosi cha Bayer Leverkusen.
Mlinzi huyo amekuwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kuingia katika rada za usajili wa Manchester City inayopanga kupambana kwa ajili ya kurejea katika mafanikio makubwa msimu ujao.
Katika kuhakikisha wanafanikisha azma hiyo, City imekuwa ikimfuatilia Boeder katika baadhi ya mechi ambazo Leverkusen inacheza ndani ya Bundesliga.
Mawakala wa City wamekuwa wakisafiri mara kwa mara hadi nchini Ujerumani kwa ajili ya kujiridhisha na kiwango cha sasa cha mlinzi huyo.
Comments
Post a Comment