BOSI wa Matajiri wa Jiji la Manchester, Manchester City, Manuel Pellegrini wala hana haja ya mustakabali wake wa ama kubaki au kuondoka.
Katika kujiaminisha kuwa bado ana nafasi ya kubaki, ndio kwanza ameanza kupanga safu ya usajili wa dirisha la majira ya joto kwa kusaka saini ya beki wa kati, Lukasz Piszczek.
City imekuwa katika mbio za kumsainisha nyota huyo kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa dau la pauni 35 mil.
Hatua ya City kutaka kumwita kundini mlinzi huyo ni kutokana na mkakati wake wa kuendelea kusuka kikosi imara cha kuipa mataji klabu.
City iliyoshindwa kutetea taji la premier msimu uliopita, ilimweka katika wakati mgumu kocha Manuel Pellegrini na sasa imepanga kuingia sokoni kusajili nyota kadhaa walio bora.
Akinukuliwa Pellegrini alisema: "Lukasz ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa walio katika kiwango cha juu na ana kipaji cha kuweza kucheza katika klabu yoyote kubwa hivyo City haipaswi kumuacha."
"Ana sifa moja kubwa, nayo ni uwezo wake wa kuwakabili washambuliaji wa timu pinzani na anajua kujipanga hasa katika mazingira magumu."
"Kizuri ambacho ni sifa yake ya ziada ni kwamba ni mzuri katika kupanga safu ya ulinzi, hivyo ni mtu muhimu kwa sasa katika kiwango cha soka la dunia," alizungumza Pellegrini na kunukuliwa na The Goal.
"Sikuwahi kumshawishi kwa kiasi kikubwa, lakini ninatambua vyema uwezo alionao ambao ni muhimu kwetu kma klabu itafanya jitihada kumpata na kuimarisha safu ya ulinzi."
"Kama atafanikiwa kutua kwetu nitajisikia furaha ya kupitiliza kwasababu ndoto ya fikra zangu itakuwa imetimia."
"Hakuna jambo la siri ukiwa unamalizana na mchezaji bora wa kiwango chake. Ni vyema kuwa na wachezaji wanne ama watano katika kikosi utakuwa umejihakikishia kikosi bora."
"Kama unaweza kusema lililo kweli ni kwamba ndani ya kikosi chetu tulihitaji wachezaji wa mfano wake ambapo ninaamini anacheza vyema na Vicent Company."
Manchester City imepanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kufanya usajili wa dirisha la Januari, huku azma ikiwa ni kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa premier ambao msimu huu umechukuliwa na Chelsea.
Comments
Post a Comment