KUNA kauli moja amezungumza Luis Suarez kuwa awali            hakuwa na ndoto ya kuweza kucheza vyema akiwa katika kikosi            kimoja na nyota wa dunia, Lionel Mess.
        Lakini tangu akiwa Barcelona na kumudu kupewa majukumu            ya kucheza kama mshambuliaji wa kati, amefarijika na hatua ya            kiwango chake cha sasa.
        Alisema, kabla ya kujiunga na Barca akitokea Liverpool            mwaka 2014 hakutarajia kucheza katika jukumu alilonalo Messi,            ingawa kwa sasa amekiri kufanikiwa.
        Suarez kwa sasa amepachika mabao 40 katika mechi 35            ambazo alipangwa msimu huu na kuingia katika orodha ya            wachezaji walio na magoli mengi akichuana na Cristiano Ronaldo            wa Real Madrid.
        Kwa nyakati tofauti, Messi amekuwa nje ya kikosi cha            Barca kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kuwa majeruhi, lakini            Suarez amekuwa akichukua nafasi yake na kucheza kama            mshambuliaji wa kati.
        "Nimekuwa nikipangwa kama namba tisa wakati Messi            hayupo ama hata akiwepo tumekuwa tukicheza kwa kubadilishana            wakati mchezo ukiendelea. Hii ni hatua ya kujivunia," anaeleza            Suarez
        "Kucheza katika mfumo wa kujiamini na kupokezana            kumeisaaidia timu kutomtegemea mchezaji mmoja katika idara ya            ushambuliaji, ndio maana utatukuta tunacheza kwa kupichana."
        "Ninaweza nikawa mimi, baadae Messi na kisha Neymar,            wote tumekuwa tukipangwa kulingana na aina ya mchezo na            tumekuwa katika mfumo mzuri siku zote," alisisitiza Suarez na            kuongeza."
        "Nimekuwa nikiwaambia kuwa watoto wangu kuwa ninacheza            katika kikosi kimoja na mchezaji nyota duniani na ni jambo la            kihistoria. Hii ni bahati na jambo la kujivunia."
        Suarez alizungumzia kwa mara nyingine tukio la kung'ata            Giorgio Chielini katika tukio lililofanyika wakati wa fainali            za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil na kuliita ni jambo            la kibinaadamu lisilopendeza.
        
Comments
Post a Comment