LOUIS VAN GAAL SASA AISHI KWA MATUMAINI


LOUIS VAN GAAL SASA AISHI KWA MATUMAINI
After being questioned            about his future for months, Van Gaal snapped ahead of            Sunday's game with Leicester

LOUIS VAN GAAL amesema "piga ua" Manchester United bado ina nafasi ya kufuzu kucheza Champions League msimu ujao licha ya kuachwa pointi nne na wapinzani wao wa mji mmoja – Manchester City iliyo juu ya mstari wa 'Top Four'. Wakati United ikiwa na pointi 60, City ina pointi 64.

Kuweza kutimiza ndoto hiyo, Van Gaal anatakiwa kushinda mechi zake zote tatu zilizobaki dhidi ya Norwich (ugenini), West Ham (ugenini) na Bournemouth (nyumbani), huku akiwaombea mabaya City waliobakiwa na mechi mbili dhidi ya Arsenal (nyumbani) na Swansea (ugenini).

"Bado tupo katika mbio za kufuzu kwa Champions League. Ni muhimu sana kwa mashabiki na wachezaji," alisema na kuongeza: "Kwa kocha, kutwaa ubingwa ni muhimu sana, lakini mimi ni kocha wa Manchester United, kwa United ni muhimu sana kucheza katika Champions League.

"Na bado inawezekana. Tunapaswa kushinda mechi tatu za mwisho na nilisema hilo kabla ya mechi dhidi ya Leicester City."





Comments