Njozi za kocha Jurgen Klopp kutwaa taji la Ulaya katika msimu wake wa kwanza Liverpool, zimeota mbawa baada ya timu hiyo kulambwa 3-1 na Sevilla katika fainali ya Europa League.
Liverpool ilikuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 35 kupitia kwa Daniel Sturridge, lakini Sevilla wakachomoa dakika ya 46 kwa bao la Kevin Gameiro.
Coke akaifungia Sevilla mabao mawili ya haraka haraka dakika ya 64 na 70 yaliyotosha kuimaliza Liverpool.
Fainali hiyo ilipigwa kwenye uwanja wa St. Jakob Park huko Basle, Switzerlandna hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Sevilla ya Hispania kutwaa taji hilo.
Daniel Sturridge akishangilia bao pekee la Liverpool
Comments
Post a Comment