STRAIKA Lionel Messi amesema kwamba anavyoamini timu ya taifa ya Argentina ndiyo inayostahili kutwaa ubingwa wa michuano ya Copa America Centenario itakayofanyika mwezi ujao nchini Marekani.
Argentina ilikosa taji hilo mwaka jana kwa mikwaju ya penati dhidi ya Chile, ikiwa ni takribani mwaka mmoja baada ya kuchapwa na Ujerumani katika mechi ya fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Ujerumani zilizofanyika nchini Brazil.
Vigogo hao wa soka uknada wa Amerika Kusini wameshatinga mara tatu kati ya nne za fainali hizo za Copa America lakini ikajikuta ikiishia kuwa mshindi wa pili na haijawahi kutwaa taji hilo tangu mwaka 1993.
Hata hivyo Messi sasa ni wakati wa Argentina kuonja ladha ya ushindi wa taji hilo, ikiwa ni baada ya kuka muda wa miaka 23 bila kutwaa taji lolote kubwa.
"Tutajaribu kufanya kila tuwezalo ili tutwae Kombe la Copa America, kwasababu kwetu sisi ni muhimu mno," staa huyo wa Barcelona aliuambia mtandao wa Sports Illustrated.
"Cha muhimu zaidi ni kwamba ni muda mrefu tangu Atrgentina ishinde taji lolote na jambo hilo lilikaribia kumalizika wakati wa fainali za Kombe la Dunia na michuano ya mwaka jana ya Copa America," aliongeza nyota huyo.
"Nadhani tunastahili kuwa mabingwa wa mashindano hayo muhimu," aliongeza tena staa huyo.
Argentina itaanza michuano hiyo kwa mechi ya kulipiza kisasi dhidi ya watakayokutana nao kwenye fainali dhidi ya Chile Juni 6, mwaka huu, kabla ya kuwavaa wapinzani wake katika kundi hilo D, Panama itakayokutana nayo Juni 10 na siku nne baadaye dhidi ya Bolivia.
Comments
Post a Comment