Hatimaye John Terry amesaini mkataba mpya Chelsea utakaomwezesha kukipiga Stamford Bridge kwa mwaka mmoja zaidi.
Terry ambaye alikuwa njiani kutundika daluga, sasa atakuwa nafasi ya kuongeza idadi ya michezo 703 aliyoichezea Chelsea aliyojiunga nayo miaka 22 iliyopita.
Habari hizi zinaondoka kabisa ukungu uliotanda juu ya hatma ya nahodha huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye alionekana kama anataka kutupiwa virago vyake.
Mwezi Januari Terry alifichua kuwa klabu haikuwa na nia yoyote ya kurefusha mkataba wake, hali iliyoonyesha kuwa ndoa ya beki huyo na Chelsea inaelekea ukingoni.
Nahodha wa Chelsea John Terry ameongezewa mwaka mmoja wa kubakia Stamford Bridge
Comments
Post a Comment