JERRY MURO AMETOA MSIMAMO WA YANGA KUHUSU TETESI ZA NGOMA KUTIMKA JANGWANI



JERRY MURO AMETOA MSIMAMO WA YANGA KUHUSU TETESI ZA NGOMA KUTIMKA JANGWANI

IMG_0307

Klabu ya Yanga imekanusha taarifa zilizoenea mtaani kwamba mshambuliaji wao raia wa Zimbambwe Donald Ngoma anataka kuihama klabu yao.

Kuna taarifa ambazo zimesambaa upitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii zikidai nyota huyo aliyefanikiwa kufunga magoli 17 kwenye msimu wake wa kwanza VPL anawaniwa na vilabu vya Misri na Afrika Kusini nay eye yuko tayari kujiunga navyo.

"Yanga bado inamkataba wa mwaka mmoja na Ngoma baada ya kumalizika kwa msimu huu. Bado hatujapokea ofa kutoka klabu yeyote inayomtaka Ngoma. Hizo ni taarifa ambazo siyo rasmi na wanachama na mashabiki wanatakiwa kuzipuuza", amesema Jerry Muro ambaye ni ofisa habari wa klabu ya Yanga.

"Ngoma anaipenda Yanga na anafurahia maisha ya Tanzania. Ameshaanza kujifunza Kiswahili na kama mwenzake Kamusoko ambaye tayari anazungumza vizuri Kiswahili, na inaashiria ni kwa kiasi gani anafurahia kuwa hapa", amesisitiza Muro.

Uwezo mkubwa uliooneshwa na Ngoma kwenye VPL, FA Cup, kombe la klabu bingwa Afrika pamoja na kombe la Shorokisho Afrika, huenda umevitoa udenda vilabu kadhaa vya nje ya Tanzania na kuanza kuisaka saini ya nyota huyo aliesajiliwa na Yanga akitokea klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe.



Comments