JACK WILSHERE AMLALAMIKIA ARSENE WENGER KUMUUA KISOKA





JACK WILSHERE AMLALAMIKIA ARSENE WENGER KUMUUA KISOKA
JACK Wilshere amemshambulia kocha Arsene Wenger kwamba anamuua kwa kumchezesha katika nafasi isiyo yake klabuni Arsenal.

Kiungo huyo, 24, amekuwa akichezeshwa katika kiungo cha pembeni kwenye klabu yake, lakini amekuwa akicheza kati zaidi katika timu ya taifa ya England.

"Klabuni Arsenal nimekuwa nikicheza pembeni, eneo ambalo si langu," Wilshere alisema.

"Mimi si winga lakini Roy (Hodgson), anaonekana kuwa na imani nami kunitumia katika eneo la kati, hivyo nina furaha katika hilo."

Kocha wa timu ya taifa ya England, Hodgson amemwita Wilshere katika kikosi cahe cha awali cha wachezaji 26 kuelekea fainali za mataifa ya Ulaya na anatarajiwa kuwemo katika wakali 23 watakaoenda Ufaransa.


Wilshere amecheza mechi tatu tu msimu mzima Arsenal wakati akipambana kurejea uwanjani kufuatia kuumia mguu, lakini Hodgson alidhamiria kumwita taifa licha ya kutocheza kiasi cha kutosha.


Comments