HECTOR BELLERIN ASEMA NI JAMBO JEMA SAINI YAKE KUWANIWA NA BARCELONA



HECTOR BELLERIN ASEMA NI JAMBO JEMA SAINI YAKE KUWANIWA NA BARCELONA

HECTOR BELLERIN amesema ni jambo zuri sana kwake kusikia kuwa Barcelona inahitaji saini yake.
Hata hivyo beki huyo wa kulia wa Arsenal amesema licha kujisikia fahari kuwaniwa na Barcelona, lakini hana mpango wa kuondoka Arsenal kwa vile anafuraha na maisha ndani ya klabu hiyo ya London.
Wakati Dani Alves akijiandaa kuondoka Nou Camp baada ya misimu nane ya mafanikio, Barcelona sasa inahaha kusaka mrithi wa Mbrazil huyo.
Bellerin, ambaye alilelewa Bracelona na kuichezea timu yao ya vijana, ndiye mlengwa mkuu wa kuziba nafasi ya Alves.
Kinda huyu wa miaka 21 alikaa miaka minane Barcelona kabla ya kuhamia Arsenal akiwa  na umri wa miaka 16.
Tangu alipopata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Arsenal pale alipoumia Mathieu Debuchy, Bellerin akaibuka kuwa tegemeo Arsenal na hatimaye kujumuishwa kwenye 11 bora  ya wachezaji wa kulipwa Ligi Kuu ya England (PFA Team of the Year) msimu uliomalizika.



Comments