KOCHA wa Chelsea, Guus Hiddink ameeleza kwamba kocha mwenzake wa Leicester City, Claudio Ranieri alimpigia simu kumshukuru mara baada ya mechi yao dhidi ya Tottenham kumalizika kwa sare ya 2-2 Jumatatu usiku.
Matokeo hayo yaliyokuja baada ya Chelsea kuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi mapumziko, yameiwezesha Leicester kuwa mabingwa wa Premier League kwa mara ya kwanza, na kuwa habari kubwa katika soka ya England.
"Mara tu baada ya mechi, baada ya filimbi ya mwisho, nilipata simu kutoka kwa Ranieri," alisema Hiddink na kuongeza kuwa kocha huyo wa Leicester alikuwa na furaha sana kwa juhudi walizoonyesha dhidi ya Spurs.
"Alitushukuru kwa tulichofanya, hasa katika kipindi cha pili. Nilimpongeza kwa kuwa bingwa… Alikuwa na hisia. Sikuona machozi kwa sababu hayakuwa mazungumzo ya ana kwa ana, lakini sauti yake ilikuwa na tetemeko kidogo, ndiyo.
"Alisema shukrani mara tano kwa sababu hisi zilikuwa zinazidi kupanda."
Comments
Post a Comment