Guardiola amefeli Bayern Munich: Messi, CR7 na Griezmann wamechangia


Guardiola amefeli Bayern Munich: Messi, CR7 na Griezmann wamechangia

Utawala wa Pep Guardiola katika klabu ya Bayern Munich angalau kwa upande wa michuano ya Champions League umefikia mwisho. Kocha huyo mkatalunya, ambaye alimrithi mshindi wa makombe matatu ya kihistoria Jupp Heynckes, ameshindwa kufikia mafanikio ya mtangulizi wake na sasa ataondoka kwenda kujiunga na Manchester City bila kutimiza ndoto yake na ya mashabiki wa Bayern ya kushinda ubingwa mwingine wa ulaya miaka 3 baada ya kujiunga na Bavarians.

  Rekodi nzuri ya makombe ilikuwa ndio ngao kuu ya kumlinda kocha huyu mwenye umri aa miaka 45 na falsafa zake za soka, ambazo zilikuwa zikiwapa mashaka na baadhi ya wadau kama vile wachezaji, mashabiki, legends kama vile Franz Beckenbauer na Karl Heinz Rummenigge.

"Tutakuja kuwa hatuangaliziki kama Barca. Hakuna atakayetaka kutuangalia, kwa sababu wachezaji watakuwa wanacheza kwa kupiga pasi za kurudi nyuma," Kaiser alisema baada ya Pep kuteuliwa kushika madaraka, kabla hajaja kubadilisha maneno na kusifu mbinu za kocha huyo wa kihispaniola.

Pamoja na kushinda Bundesliga kila msimu katika miaka yake yote pale Allianz Arena, pia kombe la ligi mwaka 2014, utawala wa Guardiola umekuwa na bahati mbaya ya kutolewa mara tatu mfululizo katika Champions League hatua ya nusu fainali na vilabu vya Hispania.

  Real Madrid walikuwa wa kwanza kuwa kizingiti cha Pep Guardiola kuingia fainali mwaka 2014 kwa kuwapa Bayern kipigo cha 0-4 @Allianz Arena. Kikosi cha Luis Enrique cha Barcelona wakafuatia kuiondoa Bayern nje ya mashindano kwa kuwafunga 3-0 Camp Nou na 3-2 Allianz Arena katika hatua ya nusu fainali.

  Hatimaye jana usiku Atletico Madrid nao wamefanikiwa kuiondoa Bayern katika nusu fainali ya michuano ya Champions League msimu huu kwa kuwafunga 1-0 Vicente Carlderon na usikua wa kuamkia leo wakafungwa 2-1 lakini wakafuzu kwa goli la ugenini.  
Katika miaka yote hii timu ambayo iliifunga Bayern huenda na kutwaa ubingwa wa ulaya, Je Atletico ataweza kuzitafuna aidha Real Madrid au Manchester City.



Comments