UHAMISHO wa Granit Xhaka kutua Arsenal              umeiva bada ya picha za mchezaji huyo akipozi kwa ajili ya              kupigwa picha kwenye uwanja wa mazoezi ya klabu hiyo wa              London Colney kuvuja.
        Kiungo huyo, 23, aliwasili London Ijumaa              iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya              kusaini mkataba wa miaka minne na Arsenal na picha za Xhaka              akiwa ametinga jezi mpya za Arsenal zitakazovaliwa msimu              ujao wa 2016/17, ambazo pia bado hazijatambulishwa rasmi.
        Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswisi              amekuwa akifuatiliwa na Arsene Wenger kwa miezi kadhaa na              baada ya kuafikiwa kwa ada ya uhamisho ya pauni mil 33.3 na              klabu  yake ya Borussia Monchengladbach, anakuwa mchezaji wa              kwanza kuwasili Arsenal katika kipindi hiki cha usajili              kinachotarajiwa kuwa 'bize'.
        Mtumiaji wa ukurasa wa Twitter, Valon              Demiri ambaye maskani yake ni Kosovo, aliposti picha hizo              kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuripotiwa kuzipata              kutoka kwa mtu wa karibu na Xhaka.
          
            
        Kiungo huyo ametua London na wazazi wake,              kaka yake na mkewe kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na              kupozi kwa ajili ya picha kabla ya kutangazwa rasmi kwa              usajili huo.
          
        
Comments
Post a Comment