GRANIT XHAKA AIFAGILIA LIGI KUU ENGLAND



GRANIT XHAKA AIFAGILIA LIGI KUU ENGLAND
STAA mpya wa Arsenal, Granit Xhaka amesema ligi ya Uingereza itamfaa kwasababu ni mchezaji mwenye nguvu na anayependa kupambana.

Arsenal Jumatano hii walitangaza kwamba wamefanikiwa kiumsajili mchezaji huyo raia wa Uswisi kutoka Borusia Monchengladbach, anayetua akitokea Bundesliga na sifa kama mchezaji mahiri katika kukaba dimbani.

"Napenda uchezaji wa Ligi ya Uingereza, ni soka la kibabe," alisema Xhaka kaytika mahojiano yake ya kwanza kwenye tovuti ya klabu.

"Ni mapambano, napenda sana lakini pia Arsenal ni klabu inayocheza mpira wa hali ya juu na hiyo ni nzuri sana."
"Katika Ujerumani utacheza soka la kibabe lakini mara nyingi mwamuzi hupuliza kipyenga lakini kwa Uingereza haiku hivyo, hii ni njema sana kwangu."

Xhaka anatarajia kuimarisha kikosi cha Arsenal ambacho kimetajwa kuwa nyororo sana, mara nyingi amefanya makabiliano 'tackle' 244 katika mechi 108 alizocheza Bundesliga.

Hata hivyo aina yake ya uchezaji imemuingiza matatizoni mara kadhaa kwani ametolewa mara tano kwa kadi nyekundu Bundesliga.


Xhaka aliiongoza Gradbach kumaliza nafasi ya nne msimu uliopita na amesema yuko tayari kupewa kitambaa cha unahodha Arsenal pia.


Comments