ERIC BAILYY AIKATA MAINI REAL MADRID




ERIC BAILYY AIKATA MAINI REAL MADRID

MLINZI wa katikati wa klabu ya Villareal ya Hispania, Eric Bailly amewaambia Real Madrid kuachana na azma yakutaka kumng'oa kwasababu bado hana sababu ya kutaka kuachana na timu yake ya sasa.

Kwa msisitizo Eric Bailly amesema kuwa anajisikia furaha na maisha ndani ya Villareal.

"Taarifa hizo za klabu nyingi kunihitaji zinanipa faraja na heshima kubwa, lakini dhamira yangu ya sasa ni kuendelea kubaki hapa kwani bado nina kandarasi ya mwaka unusu kuendelea kuwepo Villareal," alisisitiza.

Kwa sasa beki huyo mwenye umri wa miaka 21 anatajwa katika dili la usajili Real Madrid.
Madrid wametajwa katika mpango wa kuimarisha kikosi chao na Zinedine Zidane amesema Bailly ni kati ya walinzi imara wa kuwajumlisha katika kikosi cha msimu ujao.

Raia huyo wa Ivory Coast alithibitisha kusikia taarifa za kutakiwa na wakongwe hao lakini alikanusha kuhusu kukubali kujiunga nao katika majira ya kiangazi.

"Sifahamu lolote juu ya tetesi hizo japo nimezisikia," Bailly aliliambia AS.

"Ninachojua ni kwamba ninataka kumaliza kandarasi yangu nikiwa na Villareal. Hii ni klabu yangu, bado nina mkataba wa miaka miwili, nina furaha kuwa hapa."


Comments