DE GEA KUAONDOKA MANCHESTER UNITED IWAPO VAN GAAL HATATIMULIWA


DE GEA KUAONDOKA MANCHESTER UNITED IWAPO VAN GAAL HATATIMULIWA
Kipa wa MANCHESTER UNITED  David de Gea huenda akaandoka Old Trafford kiangazi hiki iwapo Louis van Gaal ataendelea kuwa kocha wa klabu hiyo msimu ujao.
Van Gaal bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake na kuna matarajio madogo kuwa atapewa nafasi ya kumaliza mkataba huo.
Ingawa Van Gaal anaamini kuwa De Gea yuko na furaha Old Trafford, lakini watu wa karibu na mlinda mlango huyo wanabainisha kuwa kuendelea kuwepo kwa Van Gaal kutafungua milango wa De Gea kutimka Manchester United.
Inaelezwa kuwa De Gea, kipa wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 25, haamini katika mfumo wa Van Gaal.




Comments