Cristiano Ronaldo amemkingia kifua kocha mpya ajaye Manchester United Jose Mourunho kwa kusema huyo ndiye mtu sahihi wa kuirejesha klabu hiyo katika enzi za kuzoa mataji.
Mourinho anakuwa kocha mpya wa United kufuatia kutimuliwa kwa Louis van Gaal na licha ya jina la Mourinho kupokelewa kwa hisia tofauti na wachambuzi wa soka, Ronaldo amewatoa shaka mashabiki wa timu yake hiyo ya zamani kwa kusema Mreno mwenzake ndiye mtu sahihi kwa sasa Old Trafford.
Ronaldo aliyetumikia United kwa miaka sita ya mafanikio makubwa, amesema Mourinho ni chaguo bora zaidi.
Manchester United inajiandaa kumtangaza Jose Mourinho kama kocha wake mpya
Cristiano Ronaldo anatumai kuwa Mourinho ataleta mataji United.
Comments
Post a Comment