KOCHA wa zamani wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amebainisha kwamba Cristiano Ronaldo anajitoa kikamilifu katika fani yake kiasi kwamba huoga na maji ya barafu alfajiri, hata kama rafikiye wa kike wa zamani, Irina Shayk alikuwa akimsubiri nyumbani.
Muitalia huyo ambaye atachukua mikoba ya kuifundisha Bayern Munich msimu ujao, ameangalia nyuma alipofanya kazi ya ukocha Real Madrid na akazungumzia tabia za kiweredi za Mreno huyo.
"Cristiano Ronaldo alioga barafu saa tisa usiku, hata kama Irina alikuwa nyumbani akimsubiri," alisema katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times.
"Hakujali kuhusu pesa; alichotaka ni kuwa bora tu."
"Siwezi kukuelezea kwa kina lakini ninachokwambia ni babkubwa kwa jinsi anavyojitoa kwa ajili ya mafanikio yake kuliko kujali vimwana wanamitindo au mambo mengine."
Comments
Post a Comment