Manchester United imepigwa kumbo la mwaka baada ya Bayern Munich kumsajili kiungo wa Benfica Renato Sanches ambaye iliaminika anakwenda Old Trafford.
Renato Sanches mwenye umri wa miaka 18, amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia Bayern Munich katika dili litakalopanda hadi kufikia thamani ya pauni milioni 63.
Hadi mwanzoni mwa wiki hii, Sanchez alikuwa akitwajwa kukamilisha safari ya kujiunga na Manchester United ambayo imekuwa ikimfuatilia kinda huyo kwa msimu mzima, lakini kwa maajabu ya wengi, Bayern Munich ikaibuka ghalfa na kumnyakua kiungo huyo mwenye kipaji cha aina yake.
Bayern Munich imetangaza kumsajili Renato Sanches kutoka Benfica kwa pauni milioni 28 - Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amesaini mkataba huo mbele ya mtendaji mkuu wa Beyern Karl-Heinz Rummenigge
Sanches akipozi na Rummenigge baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano
Sanches akifanya vipimo vya afya Bayern Munich
Comments
Post a Comment