BARCELONA NA REAL MADRID ZAPIGANA KUMBU KUWANIA SAINI YA VICTOR LINDELOF ANAYEWANIWA PIA NA MAN UNITED
KLABU mahasimu katika La Liga Real Madrid na Barcelona zimeingia katika vita ya usajili wa msimu ujao na kujikuta wakimwania kwa pamoja Victor Lindelof.
Pamoja na vigogo hao wa Ligi ya Hispania, pia Manchester United wanatajwa katika mbio hizo za kumwania nyota huyo wa klabu ya Benfica.
Mlinzi huyo kijana amekuwa katika kiwango bora katika msimu huu kiasi cha kuzigonganisha timu mbalimbali, lakini Sky Sports imezitaja Barca na Real Madrid ndio zilizoonyesha nguvu kubwa ya kupata saini yake.
Lindelof mwenye umri wa miaka 21, yumo pia katika kikosi cha timu ya taifa ya Sweden, alikuwa katika orodha ya wachezaji wanaoweza kuuzwa lakini taarifa za hivi karibuni zimesema kuwa Benfica imesitisha azma hiyo.
Imebainika kuwa Benfica imesitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada ya kuondokewa na mlinzi wao mahiri, Renato Sanches aliyejiunga na Bayern.
Katika kuhakikisha haimpotezi Lindelof, imeamua kuweka mezani ofa kubwa ya euro 40 mil ambapo imebainika klabu za Barca na Madrid zinaweza zisipande dau hilo.
Comments
Post a Comment