ATLETICO MADRID KUVUNA ZAIDI MATANGAZO YA HAKI ZA TELEVISHENI



ATLETICO MADRID KUVUNA ZAIDI MATANGAZO YA HAKI ZA TELEVISHENI
ATLETICO Madrid itakuwa miongoni mwa klabu zitakazofaidika kwa ukubwa zaidi kwenye dili jipya la uuzaji wa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za Ligi Kuu ya Hispania La Liga.

Kwa mujibu wa ripoti inaaminika kwamba Atletico walikuwa wakipata kiasi cha euro milioni 45 mpaka kufikia kiasi cha milioni 100 kwa mwaka.

Los Lojiblancos, mabingwa wa La Liga miaka miwili iliyopita bado wapo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa mara nyingine msimu huu na wamefaidika zaidi kutokana na sheria mpya za mgawanyo wa fedha ambao umetengenezwa ili kuweka usawa kwa kiasi fulani mongoni mwa klabu.

Fedha hizi zitakuza pato mpaka kuzidi mapato ya timu kama mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich ambao wanapokea kiasi cha euro milioni 50 na mabingwa wa Italia, Juventus ambao wnapokea kiasi cha euro milioni 94.

Ni klabu kubwa tu za premier league, mashindano tajiri zaidi duniani, ambao watapokea fedha nyingi zaidi ya Atletico zikiwemo Manchester United, Manchester City na Chelsea ambao watapokea kiasi cha zaidi ya euro milioni 165.


Kanuni mpya ambazo zitaanza kutumika kuanzia msimu ujao zitapunguza nguvu za Madrid na Barcelona ambao wao hupokea kiasi cha euro milioni 140 kila timu na timu nyingine kidogo kama Eibar watakuwa wakipokea kiasi cha euro milioni 43 badala ya euro milioni 18 wakati Sevilla watapokea kiasi cha euro milioni 60.


Comments