YAYA TOURE ni 'mlevi' wa magari ya            kifahari na sasa amewafunika mastaa wenzake wa Manchester City            katika eneo la maegesho ya magari la klabu hiyo akiwa na Rolls            Royce mbili zenye thamani ya jumla ya pauni 600,000.
        Kiungo huyo raia wa Ivory Coast mwenye            miaka 32, tayari alikuwa na Rolls Royce Wraith yenye thamani            ya pauni 250,000 lakini akafunikwa na Samir Nasri aliyenunua            Lamborghini Aventador kwa pauni 330,000.
        Sasa Toure amefungua tena pochi yake na            kununua Rolls Royce Phantom kwa pauni 350,000 na kumfanya            kumiliki magari ya kifahari yenye thamani ya jumla ya pauni            milioni 1.
        Miezi 12 iliyopita, Toure ambaye            anahusishwa kuondoka Etihad kiangazi hiki, alionekana            akiendesha Mercedes G Class jeep yenye thamani ya pauni            150,000, Mercedes Brabus 850 ya pauni 300,000, Bentley            Continental ya pauni 200,000 na Porsche Carerra ya pauni            90,000.
        Staa huyo anayelipwa mshahara wa pauni            220,000 kwa wiki, Jumatatu wiki hii ameonekana akiendesha            Rolls Royce Phantom nyeusi akielekea mazoezini.
        
Comments
Post a Comment