LOUIS VAN GAAL amefurahi "kuona furaha" katika macho ya wachezaji wake na mashabiki wa Manchester United baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton katika nusu fainali ya FA Cup iliyopigwa Wembley Jumamosi jioni.
Akizungumza na BBC Sport baada ya filimbi ya mwisho, Van Gaal alisema: "Wakati unapoona furaha katika macho ya wachezaji, ni nzuri sana, lakini pia kwa mashabiki. Nadhani tulistahili kwenda katika fainali."
Hata hivyo kocha huyo alisema kuwa hakufurahishwa na refa kwa jinsi alivyochezesha mechi hiyo kwamba alibadili mchezo kwa "kuwanyima faulo".
Anthony Martial alifunga mwishoni kumaliza mchezo baada ya awali kumtengenezea nafasi Marouane Fellaini kuipa United uongozi wa 1-0.
Everton walipoteza penalti wakati ubao ukionyesha wako nyuma kwa 1-0, baada ya David De Gea kuokoa shuti la Romelu Lukaku, lakini wakafanikiwa kusawazisha kwa Chris Smalling kujifunga kabla Martial kuwaliza.
Comments
Post a Comment