WAARABU WAJITOSA KUINUNUA LIVERPOOL



WAARABU WAJITOSA KUINUNUA LIVERPOOL
The Liverpool players            celebrate after 21-year-old Divock Origi converted James            Milner's cross just minutes before the half-time whistle

LIVERPOOL inatarajiwa kuingia katika orodha ya klabu za Premier League zinazomilikiwa na mabilionea wa Kiarabu.

Tayari Manchester City inamilikiwa na Sheikh Mansour bin Zayed bin Sultan bin Zayed bin Khalifa Al Nahyan, maarufu kama Sheikh Mansour anayetoka katika familia ya kifalme inayotawala Abu Dhabi, ambaye ni Naibu Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Waziri wa Mambo ya Rais.

Sasa mmoja wa wanafamilia hiyo, ameripotiwa kujiandaa kuinunua Liverpool na tayari ana zaidi ya pauni milioni 700 benki zikisubiri kukamilisha dili hilo.

Ingawa utambulisho wa mtu anayetaka kuinunua klabu hiyo umebaki kuwa siri, taarifa zinamtaja Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Khalifa bin Zayed bin Sultan Al Nahyan, aliye maarufu kwa jina la Sheikh Khalifa ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya zaidi ya pauni bilioni 30.

Sheikh Khalifa ni kaka wa Sheikh Mansour ambaye ameigeuza City kuwa mabingwa mara mbili wa Premier Leagu tangu alipoinunua mwaka 2008.

Mtandao wa Starsport ulibainisha mwanzoni mwa mwezi kwamba mazungumzo tayari yameanza juu ya mapendekezo ya kuuzwa kwa klabu hiyo.

Liverpool ina thamani ya pauni karibu milioni 650 na kwa sasa inamilikiwa na Kampuni ya uwekezaji ya michezo ya Marekani, Fenway Sports Group (FSG) iliyoinunua kwa pauni milioni 300 Oktoba 2010.


Comments