Taji la FA linaweza likampa faraja kocha wa Machester United Louis van Gaal, lakini inaaminika halitamwokoa katika kupigania kibarua chake Oldt Trafford.
United inajitupa kwenye dimba la Wembley hapo baadae kuchuana na Everton katika nusu fainali ya FA Cup na ingawa kikosi cha Van Gaal kinapewa nafasi kubwa ya ushindi, lakini ni nafasi ya nne kwenye Top Four ya Premier League ndiyo inayoweza kumwokoa kocha huyo wa Uholanzi.
Wachambuzi wa soka England wanaendelea kumuhusisha kwa kiasi kikubwa kocha Jose Mourinho na kibarua cha kuikochi United msimu ujao.
Van Gaal amekuwa akijipa moyo kutokana kuimarika kwa ubora wa kikosi chake, lakini bado ana kazi kuwa ya kuishawishi bodi ya Manchester United isimuonyeshe mlango wa kutokea.
Kocha huyo amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa miaka mitatu Old Trafford.
Nahodha Wayne Rooney akipokea maelekezo ya kocha wa Manchester United kabla ya kuelekea kwenye mchezo wa FA dhidi ya Everton
Comments
Post a Comment