TOTTENHAM YAITENGEA UBINGWA LEICESTER CITY …yalazimishwa sare na West Brom …Man United na Chelsea ‘kumtangaza’ bingwa Jumapili na Jumatatu ijayo
TOTTENHAM            imeitengea ubingwa Leicester City. Ndivyo unavyoweza kusema baada klabu            hiyo kushindwa kuutumia vema uwanja wake wa nyumbani White Hart Lane na kulazimishwa sare ya 1-1 na West Bromwich katika mchezo wa Ligi Kuu ya            England.
        Mchezaji Craig Dawson wa West Bromwich ndiye aliyefunga magoli yote            mawili ambapo alianza kwa kujifunga dakika ya 33 kabla hajawa            shujaa kwa kuisawazishia timu yake dakika ya 73.
        Leicester sasa            inaweza ikatwaa ubingwa Jumapili iwapo itafunga Manchester            United, lakini hata ikipoteza mechi hiyo bado itahitaji pointi            tatu tu katika michezo yake itakayofuta ili kufikisha pointi            79 ambazo ambazo hazitafikiwa na Tottenham yenye pointi 69.
        Timu zingine zote            zilizosalia zimeshapoteza nafasi ya kutwaa ubingwa, jambo            ambalo pia liko njiani kutokea kwa Tottenham.
        Tottenham            ilihitaji ushindi katika mchezo dhidi ya West Bromwich ili kuendelea kuipumulia Leicester City.
        Leicester City pia itakuwa na nafasi ya kutwaa            ubingwa hata kama itafungwa na United Jumapili halafu Tottenhm            ikafungwa na Chelsea Jumatatu ijayo.
        Boaz Myhill cannot              prevent the balls slipping through his legs after Craig              Dawson had forced it towards his own goal to put Spurs ahead
        Jan Vertonghen wa              Tottenham (katikati)anashangilia baada kumpa presha Dawson              hadi akajifunga
        Dawson anaruka juu ya              mabeki wa Tottenham na kufunga tena lakini safari hii ni bao              la kusawazisha kwa timu yake West Brom 
                    Msimamo wa ligi ulivyo 
            
          
Comments
Post a Comment